Saturday, January 21, 2017

LIVERPOOL YABANWA LIGI KUU UINGEREZA

Matumaini ya Liverpool yazimwa na Swansea

Swansea yailaza Liverpool 3-2
Klabu ya Swansea imepanda na kujiondoa katika mkia wa ligi ya Uingereza baada ya kuicharaza Liverpool 3-2 katika uwanja wa Anfield.
Gylfi Sugurdsson alifunga akiwa karibu na goli ikiwa imesalia dakika 16 na kuipatia timu ya Paul Clement ushindi wake wa kwanza tangu ajiunge na Swansea.
Roberto Firmino alifunga mara mbili na kusawazisha baada ya Fernando Liorent kufunga mabao mawili katika kipindi cha dakika nne baada ya kipindi cha kupumzika.
Ushindi huo wa Swansea unaiwacha Liverpool ikiwa nyuma ya Chelsea kwa pointi saba.

No comments:

Post a Comment