Friday, January 20, 2017

DIMBA JIPYA LA TOTTNHAM LITAKAVYOKUWA LITAKAPOKAMILIKA 2018

Tottenham Hotspur: Picha za uwanja mpya zatolewa

Image of new Spurs stadium
SpursKlabu ya Tottenham Hotspur ya Uingereza imetoa picha za kwanza za uwanja wa klabu hiyo ambao unaendelea kujengwa kaskazini mwa London.
Uwanja huo, ambao utatoshea mashabiki 61,000, utakuwa ndio mkubwa zaidi wa soka katika jiji kuu la London utakapofunguliwa mwaka 2018.
Miongoni mwa mengine, utakuwa na baa kubwa zaidi ya kuhudumia watu wote uwanjani Uingereza. Aidha, viti vyake vitakuwa na mitambo ya kubadili viwango vya joto.
Kutakuwa pia na kiwanda kidogo cha kutengeneza pombe na pia kiwanda kidogo cha kuoka mikate na keki.

No comments:

Post a Comment