Tuesday, January 17, 2017

VAN GAAL ASTAAFU UKOCHA

Van Gaal astaafu baada ya miaka 26

Van Gaal
Meneja wa zamani wa Manchester United na Uholanzi Louis van Gaal amesema amestaafu kazi ya ukufunzi baada ya miaka 26 katika taaluma yake.
Van Gaal, 65, hajafanya kazi uwanjani tangu alipopigwa kalamu na United saa chache baada ya kushinda kombe la FA mwezi Mei 2016.
"Kwa fikra yangu nilidhani nitastaafu, nikafikiria ni mapumziko ya muda, lakini kwa hivi sasa sidhani kama nitarudi kwa kazi ya ukufunzi," Van Gaal alinukuliwa na gazeti la Uholanzi la De Telegraaf.
Van Gaal pia alikuwa mkufunzi wa klabu ya Ajax, Barcelona, Bayern Munich na  AZ.

No comments:

Post a Comment