Wasafiri wa magari yaendayo Mkinga, Horohoro na Maramba kituo
cha Mwembemawazo Tanga wakiwa hawajui hatima yao baada madereva kugoma kupinga
amri ya jiji kukifunga kituo hicho badala yake kutakiwa kuanza safari zao kituo
kikuu cha mabasi yaendayo Mikoani cha Kange.
Hatua hiyo imekuja baada ya magari kutakiwa kuanza safari zao kituo kikuu ca Kange jambo ambalo madereva wamedai kuwa huko ni usumbufu kutokana na kuwa abiria wengi wa Wilayani huishia mjini ambako wengi wao ni wafanyabiashara ndogondogo (Wajasiriamali) hivyo kuwenda kwao Kange ni kuwaongezea gharama ambazo zinaweza kuwarudisha nyuma kimapato.
Madereva wa magari yaendayo Wilayani, Mkinga, Horohoro na Maramba Tanga wakiwa wamegoma kutoa magari yao baada ya halmashauri ya jiji kukifunga kituo cha magari ya abiria cha Mwembemawazo na kutakiwa kuanzia safari zao kituo kikuu cha mabasi yaendayo Mikoani cha Kange Tanga.
No comments:
Post a Comment