China yaionya Marekani kuhusu visiwa vinavyozozaniwa
Kuizuia China
katika kisiwa ilichojenga katika maji yanayogombaniwa huenda
kukasababisha mvutano mkubwa, kituo cha habari cha serikali ya China
kimsema.
Majibu hayo ya hasira yanajiri baada ya waziri mteule wa
maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson kusema kuwa Marekani
inapaswa kuizuia Beijing kuingia katika visiwa vipya katika bahari ya
kusini mwa China. .Jarida la Global Times limeonya kwamba hatua kama hiyo inaweza kusababisha vita vikubwa.
Beijing imekuwa ikitengeneza visiwa katika miamba ya maji yanayogombaniwa na mataifa mengine.
Picha zilizochapishwa mwaka uliopita zinaonyesha ulinzi mkali katika baadhi ya visiwa hivyo.
BBC
No comments:
Post a Comment