Apotea njia na kuendesha baiskeli siku 30
Mtu mmoja
nchini China ambaye alikuwa na matumaini ya kuendesha baiskeli hadi
nyumbani kwao kusherehekea mwaka mpya, aligundua baada ya siku 30 kuwa
alikuwa amepotea njia.
Mtu huyo alikuwa na matumaini ya
kuwasil nyumbani kwao huko Qiqihar mkoa wa Heilongjian baada ya kuanzia
safari yake huk Rizhao umbali wa kilomita 1,700.Lakini alisimamishwa na polisi wa trafiki akiwa amepotea umbali wa kilomita 500 katika mkoa wa Anhui.
Wakati waligundua, polisi walimlipia tikiti ya treni ili arudi nyumbani.
Ripoti zinasema kwa mwanamume huyo alikuwa akilala maduka ya intaneti kwa sababu hakuwa na pesa.
Pia hakuwa na uwezo wa kusoma ramani na hivyo alikuwa akitegemea watu kumuelekeza.
Polisi walimsimamisha kwa sababu alikuwa akitumia barabara ambayo baiskeli haziruhisiwi kuitumia.
Baada ya kugundua makosa yake, polisi na watu wote waliokuwa kituoni ambapo alisimama walichanga pesa na kumnunulia tikiti ili asafiri nyumbani.
No comments:
Post a Comment