Saturday, January 21, 2017

KOCHA KUHA IDD KUHA ANOGEWA NA USHINDI WA MABAO 2



Tanga, KOCHA wa timu ya Wanawake Queen Fair Play ya Tanga  inayoshiriki ligi kuu ya Wanawake Tanzania Bara, Kuha Idd Kuha, amesema licha ya kushinda mabao mawili dhidi ya Viva ya Mtwara timu yake haikucheza vizuri.
Akizungumza mara baada ya kipenga cha mwisho, Kuha, alisema vijana wake walicheza chini ya kiwango hivyo kusema ushindi huo wa amabao 2 , 1 mbele ya washabiki wa nyumbani sio wa kujivunia.
Alisema kipindi cha kwanza wapinzani wao walicheza vizuri mbali ya kutangulia kufunga mabao yote mawili kupitia kwa mshambuliaji wao, Mgeni Ramadhani ambapo goli la pili lilipatikana kwa njia ya Penalti.
“Siwezi kujitapa mbele ya washabiki wako katika uwanja wa nyumbani  kuwa nimeshinda ushindi wa mabao wawili, kwa kweli sijafurahi labda ningeshinda mabao manne” alisema Kuha na kuongeza
“Wenzetu waliuanza mchezo kwa nguvu ila bahati haikuwa yao ila nasi kipindi cha pili tuliwakamata sana ila bahati haikuwa yetu na ndio nikasema kuwa sifurahii ushindi wa mabao mawili” alisema
Kuha alisema wanarejea kambini kutafakari ushindi huo aliodai kuwa ni mwembamba ili kuweza kufanya vizuri katika michezo mengine ambayo iko mbele yao.
Kwa upande wake Kocha msaidizi  wa Viva Queen Fair Play, Mdanya Mkoloma, alisema anakubaliana na kipigo hicho na hana wa kumlaumu kwa madai kuwa kila mchezaji uwanjani alijituma ila bahati haikuwa yao.
Alisema wapinzani wao walicheza vizuri zaidi ya wao ila kipindi cha kwanza wachezaji wake hawakuwa makini baada ya kupata nafasi mbili za wazi za kufunga.
“Kipigo cha mabao mawili sina wa kumlaumu ila naweza kusema kuwa sote tunapaswa kujilaumu hasa kipindi cha kwanza ambacho tulicheza vizuri zaidi ya wenyeji” alisema Mkoloma
Mkoloma alimpongeza mchezaji wake alielipatia bao pekee, Fikirini Jumbe kwa bao safi ambalo amesema linaweza kuwa bao bora hadi sasa katika ligi hiyo.
                                       Mwisho



 Wachezaji wa timu ya Wanawake ya Queen Fair Play ya Tanga inayoshiriki ligi kuu ya Wanawake Tanzania Bara, wakigombania mpira na timu ya Viva ya Mtwara  katika uwanja wa Mkwakwani juzi, Queen Fair Play ya Tanga ilishinda kwa mabao 2, 1.
 Mchezaji wa Queen Fai Play ya Tanga, Emili Isaya, akiwatoka mabeki wa timu ya Queen Viva ya Mtwara wakati wa mchezo ligi kuu ya Wanawake Tanzania Bara uwanja wa Mkwakwani juzi, Fair Play ya Tanga ilishinda mabao 2, 1.
  Kiungo wa timu ya Wanawake ya Viva Fair Playa ya Mtwara, Zulfa Mwaya (17) , akimdhibiti beki wa Queen Fair Play ya Tanga, Maria Athanas  (7), wakati wa mchezo ligi kuu ya wanawake Tanzania Bara uwanja wa Mkwakwani juzi, Fair Play ya Tanga ilishinda mabao 2, 1.
Wachezaji wa timu ya wanawake  Queen Viva kutoka Mtwara inayoshiriki ligi kuu ya wanawake Tanzania Bara, wakiondosha hatari katika lango lao wakati walipocheza na timu ya Fair Play ya Tanga juzi, Fair Play ya Tanga ilishinda kwa mabao 2, 1.

No comments:

Post a Comment