Uhamiaji Marekani: Mameya wampinga Donald Trump.
Mameya wa miji
mingi nchini Marekani wanaowahifadhi wahamiaji haramu wamesema kuwa
hawatatishwa na mpango wa rais Donad Trump kupunguza ufadhili wa kieneo
iwapo hawatashirikiana naye katika mpango wake wa kutilia mkazo sheria
za uhamiaji.
Meya wa mji wa New York Bill de Blasio amesema kuwa ataupinga mpango huo wa rais na kwamba ana ushahidi wa kutosha wa kisheria.Meya wa Boston Marty Walsh amesema kuwa agizo hilo linawalenga moja kwa moja raia wa Boston na maadili yao na kuongezea kwamba atawahifadhi wahamiaji ndani ya ukumbi wa mji iwapo inawezekana.
Meya wa mji wa Seattle Ed Murray amesema kuwa mji wake hautashurutishwa na amewaagiza maafisa wake kuangazia bajeti yao upya ili kukabiliana na hatari yoyote ya kupunguziwa ufadhili.
BBC
No comments:
Post a Comment