Tanga, KILIO cha muda mrefu cha wakazi wa
Pemba na Tanga cha usafiri wa majini kimepata muarobani baada ya kampuni ya
usafirishaji abiria na mizigo ya Azam Sealink 2, kuanzisha safari yake kwa mara
ya kwanza juzi.
Usafiri huo utakuwa chachu kwa abiria na wafanyabiashara wa
Tanga na Zanzibar ambao awali walikuwa wakitumia usafiri ambao sio salama na
baadhi ya nyakati kutokea maafa na mizigo kuzama baharini .
Akizungumza na waandishi wa habari, meneja wa meli hiyo ya Azam Marinelink2, Hussein Said, amesema kilio
cha Wanzanzibar hususani wakazi wa Pemba na Tanga wakiwemo wafanyabiashara
kilikuwa kinawasononesha.
Alisema meli iko na uwezo wa kuchukua watu zaidi ya 2,000
waliokaa katika viti na shehena ya mizigo pamoja na ubebaji wa magari.
“Kwa muda mrefu kilio cha wafanyabiashara na wasafiri kwa
upande wa Tanga na Pemba tulikuwa tunajua ila muda muafaka ulikuwa bado, leo
hii niseme kuwa muarobaini wake umepatikana” alisema Said na kuongeza
“Ujio huu wa meli utafufua uchumu na biashara kwa pande zote mbili na Serikali
kuongeza mapato yake hasa kuelekea ujengaji wa bomba la mafuta ambapo kuna
fursa nyingi” alisema
Kwa upande wake mmoja wa wasafiri hao kutoka Pemba aliewasili
kwa mara ya kwanza kwa kutumia meli hiyo, Ali Makame, amesema meli hiyo itakuwa
mkombozi wa watu wa Pemba waishio Tanga na wafanyabiashara wa Tanga Pemba.
Alisema awali walikuwa wakitumia usafiri wa mashua ambao sio
rasmi na baadhi ya nyakai kulazimika kupitia Unguja hadi Dar es Salaam ambako
hutumia gharama kubwa.
“Ujio wa usafiri huu niseme kuwa ni mapinduzi makubwa kwa
wasafiri wa majini kati ya Tanga na Pembao ambao tulikuwa tunahatarisha uhai
wetu mikononi” alisema Makame
Aliyataka makampuni mengine kujitokeza hasa kipindi hiki cha
ujio wa bomba la mafuta ambapo wafanyabiashara na wawekezaji wataweza kufika na
kuangalia fursa za uwekezaji Tanga.
Abiria kutoka kisiwani Pemba wakishuka kwenye meli ya Azama Sealink2 iliyotia nanga kwa mara ya kwanza katika bandari ya Tanga juzi.
Moja ya vyumba vya VIP na viti vyake katika muonekano wake.
Life Jarket zikiwa zimehifadhiwa katika moja ya vyumba katika meli hiyo
No comments:
Post a Comment