Thursday, January 26, 2017

MLANDIZI QUEEN YAKUBALI MATOKEO TANGA, YAPIGWA 3



Tangakumekuchablog
Tanga, KOCHA Mkuu wa kikosi cha timu ya Wanawake ya Mlandizi Queen inayoshiriki ligi kuu ya Wanawake Tanzania Bara, Hussein Kyoma, amekipongeza kikosi chake kwa kutandaza soka safi mbali ya kufungwa mabao 3 kwa 1 na Queen Fair Playa ya Tanga.
Akizungumza mara baada ya kuisha kwa mchezo huo, Kyoma, alisema hana wa kumlaumu na kudai kuwa wachezaji wake wote walicheza vizuri zaidi ya wapinzani wao lakini bahati haikuwa yao.
Alisema kipindi cha kwanza wachezaji wake walicheza vizuri zaidi kwa kutumia mfumo wa pasi fupifupi na kudai kuwa wapinzani wao walipoona wanachachafya walibadilisha na kutumia mipira mirefu.
“Tumepoteza mchezo kwa kufungwa mabao matatu lakini binafsi naweza kusema kuwa ni ushindi kwani vijana wangu walicheza vizuri zaidi ya wao” alisema Kyoma na kuongeza
“Wakati mchezo tunauanza wapinzani wetu tuliwachanganya na ukiangalia mabao yao yote ni ya bahati kwani kwenye mabao matatu mawili ni ya penati hivyo naweza kusema mpira ulikuwa  droo” alisema
Kocha huyo aliwataka wachezaji wake kusahau matokeo hayo na badala yake wajipange kwa michezo iliyoko mbele yao na kusema kuwa yuko na imani na kikosi hicho na hana fikra ya kufanya usajili.
Kwa upande wake kocha wa timu ya Queen Fair Play ya Tanga, Kuha Idd Kuha, alisema ushindi dhidi ya Mlandizi Queen ni ushangiliani wa washabiki hivyo kuwataka kuendelea kujitokeza kwa wingi na kuwashangilia.
Alisema toka mashindano hayo yalipoanza hajaona washabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani na kuishangilia kwa nguvu hivyo inaonyesha kuwa  kandanda wanalotandaza linakubalika.
“Niseme kutoka moyoni kuwa ushindi ule ni hamasa ya wachezaji kwa kushangiliwa kwa nguvu na washabiki waliojitokeza si wanawake wala wanaume na wazee wa rika mbalimbali waliojitokeza kuipa nguvu timu yao” alisema Kuha
Alisema mchezo huo wapinzani kipindi cha kwanza walitawala ila kipindi cha pili baada ya kufanya mabadiliko madogo waliwakaba wapinzani wao mbali ya kuwa nao walikuwa wakitumia nguvu kubwa kusaka magoli.
Akizungumzia usajili kocha huyo alisema kuna mabadiliko madogo katika usajili ambayo atayafanya ambayo hataathiri wachezaji wengine ndani ya timu.
                                           



 Kikosi cha Mlandizi Queen Fair Play Cha Mlandizi Mkoani Pwani kikitoka uwanjani kwa huzuni baada ya kupigwa mabao 3,

 Washabiki wa mechi kati ya Mlandizi Queen na Fair Play ya Tanga wakifuatilia mechi kwa umakini



 chezaji wa Mlandizi Queen Fair Play, akiwatoka wachezaji wa Fair Playa ya Tanga wakati wa mchezo ligi kuu ya Wanawake Tanzania bara uwanja wa Mkwakwani juzi, Fair Playa ya Tanga ilishinda kwa mabao 3 , 1.
3240, Mchezaji wa Fair Play ya Tanga, Blendina Amross akigombea mpira na mchezaji wa Queen ya Mlandizi, Jamila Hassan, wakati wa mchezo ligi kuu ya Wanawake Tanzania Bara uwanja wa Mkwakwanmi juzi, Fair Play ya Tanga ilishinda kwa mabao 3 , 1.
 Kiungo wa Mlandizi Queen Fair Play, Zainab Mlenda, akimdhibiti mchezaji wa Fair Play ya Tanga, Aisha Shaban, wakati wa mchezo ligi ya Wanawake Tanzania Bara uwanja wa Mkwakwani juzi, Fair Play ya Tanga ilishinda kwa mabao 3, 1.

No comments:

Post a Comment