Monday, January 23, 2017

MKATE UNAWEZA KUSABABISHA SARATANI, WATAALAMU

Mkate tosti unaweza kuchangia saratani, wataalamu wameonya

TostiMkate, chipsi na viazi pamoja na vyakula vingine havifai kuchomwa au kupikwa hadi kupata rangi ya hudhurungi, wataalamu wameonya.
Badala yake, wanasema zinafaa kupikwa hadi viwe na rangi ya manjano iliyokolea dhahabu.
Wanasema hilo litapunguza ulaji wa kemikali ambayo huenda inachangia saratani.
Acrylamide huzalishwa wakati vyakula vyenye wanga vinapochomwa au kukaangwa kwa muda mrefu katika kiwango cha juu sana cha joto.
Wakala wa Viwango vya Ubora vya Chakula Uingereza (FSA) anapendekeza wapishi wafuate vyema maagizo wakati wa kupika na wasiache chakula kipate rangi ya kahawia.
Shirika la kukabiliana na kansa la, Cancer Research UK, linasema hata hivyo kwamba uhusiano wa moja kwa moja kati ya Acrylamide na saratani miongoni mwa binadamu haujathibitishwa.
FSA wanasema pia kwamba viazi na mboga aina ya karoti ziitwazo parsnips hazifai kuhifadhiwa kwenye friji.

No comments:

Post a Comment