Thursday, April 14, 2016

MACHINGA COMPLEX

Mwenendo wa Jengo la Machinga Complex umesababisha Waziri wa Magufuli kutoa maamuzi haya

April 14 2016 yamefanyika maadhimisho ya Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania ambapo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simbachawene amepata fursa ya kuzungumza na akatoa tamko la kuifuta na kutoitambua bodi inayosimamia jengo la machinga complex lililopo Ilala, Dar es salaam ambalo imedaiwa lilijengwa kwa ajili ya matumizi ya wafanyabiashara wadogo lakini limeonekana kutumika tofauti na kusudio hilo.
Waziri Simbachawene amelikabidhi Jengo hilo kwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuwaingiza wafanyabishara bila masharti huku ukiangaliwa utaratibu mpya kwa wafanyabiashara hao pia amewataka watumishi wa jengo hilo kuondoka mara moja na kutafuta kazi nyingnine.
Aidha Waziri Simbachawene ameziagiza halmashauri zote nchini kutotoa vibali vya leseni za biashara kwa wafanyabiashara wa kigeni hadi tamko litoke Wizarani kwake. Lengo likiwa ni kuongeza nafasi kwa wafanyabiashara wa nyumbani.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment