Tangakumekuchablob
Tanga, NAIBU
Waziri wa Nyumba na Makaazi, Angelina Mabula, amewagiza wakuu wa Idara Idara na
Taasisi za Serikali kuacha mazoea ya kutatua migogoro wakiwa maofisini na
kuwaagiza kuwa tabia hiyo ikomeshwe mara moja.
Akizungumza na viongozi mbalimbali
Idara ya Mipango miji na Shirika ;la Nyumba la Taifa leo, Mabula alisema kuna
baadhi ya wakuu wa Idara wameshindwa kubeba dhamana ya kuwahudumia wananchi na
kujikalia maofisni.
Alisema tabia ya kutatua migogoro ya
wananchi maofisni ikomeshwe na kuwataka wakuu hao kufuata kero za wananchi
sehemu husika.
Akizungumzia baadhi ya watendaji
kujipangia kazi muda kuisha na kuomba
pesa za ziada, Mabula alisema tabia hiyo ikomeshwe na kila mtu kufanya kazi kwa
kuwahudumia wananchi hata usiku.
Alisema kuna baadhi ya watendaji
wamekuwa wakijipangia kazi baada ya muda kutoka maofisini na kujilipa pesa
jambo ambalo amesema hataki kulisikia tena .
Mwisho
Katibu Tawala msaidizi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Monica Kinara, akisoma Taarifa ya Mkoa juu ya hali ya Migogoro ya Ardhi, masamba na Viwanja leo ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maakazi, Angelina Mabula (kushoto) akimsikiliza
Katibu Tawala Msaidizi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Monica Kinara,
akisoma taarifa ya Mkoa ya migogoro na changamoto ya ardhi wakati wa
ziara yake Leo.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment