Tanga, WATOTO saba wamezaliwa mkesha wa
Mwaka Mpya hospitali ya Rufaa ya Bombo Tanga mmoja kati yao akiwa wa kiume
ikiwa ni idadi pungufu ya mkesha wa mwaka jana.
Akizungumza na waandishi wa habari wodi ya wazazi Leo,
Muuguzi wa zamu, Halima Rico, alisema awali walidhani wangepokea idadi kubwa ya
wazazi na kuwa walikuwa wamejipanga vya kutosha.
Alisema mara nyingi vipindi vya mikesha ya Sikukuu huongezeka
wajawazito katika vituo vya aafya na hospitali na kwa kulitambua hilo huwa
wanajipanga.
“Mkesha wa mwaka huu tumezalisha watoto saba na mmoja kati
yao ni wakiume, hii ni tofauti na mwaka jana ambapo idadi ilizidi zaidi ya
kumi” alisema Ricco na kuongeza
“Jambo ambalo tunalishukuru wazazi wote afya zao ni nzuri
pamoja na watoto wao na kulikuwa hakuna wa upasuaji, ila jambo ambalo
limejitokeza ni kuwa kati ya saba waliozaliwa mmoja tu ndio wa kiume” alisema
Akizungumza na wazazi mara baada ya kutoa zawadi ya miche
mitatu ya sabuni kwa kila mzazi, Katibu Tawala Mkoa, Zena Said, aliwataka
wazazi kuwa na ada ya kuhudhuria kliniki ili kujua tarehe zao.
Alisema kuna baadhi ya wajawazito wamekuwa hawana ada ya
kuhudhuria kliniki hivyo kuwa na wakati mgumu wakati wa kujifungua.
“Tuko miongoni mwetu hatuna ada ya kuhudhuria kliniki jambo
ambalo linawakwaza mauguzi wakati wa kujifungua” alisema Zena
Zena aliwatakia kila la heri wazazi na watoto wao waliozaliwa
mkesha huo wa mwaka mpya na kulitakia Taifa lidumu katika amani na utulivu ili
kila mmoja afanye kazi zake za kujiletea maendeleo.
Tanga na maeneo ya jirani wakiogelea Beach ya Raskazone kusherehekea mwaka mpya Leo.
No comments:
Post a Comment