Tangakumekuchablog
Tanga,KOCHA Mkuu
wa Coastal Union ya Tanga, Ali Jangalu, amewataka wachezaji wake kujituma
uwanjani ili kuweza kupata ushindi mfululizo katika kipindi cha ligi ya lala
salama.
Akizungumza mara baada ya kumalizika
mazoezi uwanja wa Mkwakwani jana, Jangalu, alisema kila mchezaji anatakiwa
kujua wajibu wake uwanjani na kusema kuwa siri ya mafanikio ni kucheza kwa
kuelewana.
Aliwataka wachezaji hao kufanya
mazoezi mfululizo kwa kujituma asubuhi
na jioni kwa madai kuwa muda huu sio wa kulala kwani ndio kipindi cha kujua mbichi
na mbivu,
“Hadi sasa sina majeruhi na vijana
wangu wameiva na wako tayari kupambana na timu yoyote iliyoko mbele yao na
wamedhamiria kuibu na ushindi kila mchezo ulio mbele yao” alisema Jangalu na
kuongeza
“La furaha kwangu nikuwaona
wachezaji wangu wote wako fit na wanajituma katika mazoezi na wamedhamiria kushinda
mchezo na Mbeya City mwishoni mwa wiki na ninasema tutashinda” alisema
Alisema hadi sasa hakuna majeruhi
kuanzi kipa hadi washambuliaji hivyo kuwataka washabiki wa timu hiyo kuwaunga
mkono katika mechi zao zilizo mbele yao.
Aliwataka kuwashangilia kwa nguvu
katika mechi zote za ugenini na nyumbani
ili kuweza kupata ushindi mnono na kuweza kujiweka nafasi nzuri ya kubakia
kucheza ligi msimu ujao.
Mwisho
Kocha Mkuu wa Coastal Union ya Tanga, Ali Jangalu akiwaangalia vijana wake wakipita mbele yake mara baada ya kumaliza mazoezi uwanja wa Mkwakwani.
No comments:
Post a Comment