Breaking: Mahakama Dar imewaachia huru aliyekuwa Mkurugenzi wa Tanesco William Mhando na mkewe
         
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), William Mhando, mke wake Eva Mhando,
 walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es 
Salaam wakikabiliwa na mashitaka sita ikiwemo matumizi mabaya ya 
madaraka, kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Mhando 
alikuwa anatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka kwa kuipa zabuni 
Kampuni ya Santa Clara Supplies Ltd huku akijua ana maslahi nayo na 
kwamba anaimiliki yeye, mke na watoto wake. 
April 14 2016 Mahakama
 ya Hakimu mkazi kisutu Dar es salaam imemuachia huru baada ya kuona 
hana hatia kwa kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibisha juu ya 
matumizi mabaya ya ofisi na ughushaji wa nyaraka ambao inadaiwa na 
maafisa wa serikali kuwa kampuni hiyo ilifanya hivyo ili kupewa zabuni 
ambayo ilitaka kupewa na bodi hiyo ya Tanesco 
Mahakama 
imesema Mhando alikuwa haingii kwenye vikao vya maamuzi ya bodi ya 
Tanesco kwa hiyo alikuwa hana ushawishi wa moja kwa moja kushawishi 
kwamba kampuni hii ya Santa Clara ambayo ni ya mke wake kwamba ipatiwe 
zabuni.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog 
No comments:
Post a Comment