Fifa yaongeza nchi zinazocheza Kombe la Dunia hadi 48
Shirikisho la Soka Duniani Fifa limeidhinishwa mpango wa kupanua Kombe la Dunia liwe linashirikisha mataifa 48.
Mpango huo utaanza kutekelezwa Kombe la Dunia la 2026, na unatarajiwa kufaidi Afrika na Asia.Chini ya mpango ulioidhinishwa, kutakuwa na makundi 16 ya mataifa matatu kila kundi, ambapo mataifa mawili bora yataingia hatua ya muondoano ya timu.
Mpango huo ambao umekuwa ukipigiwa debe na rais wa shirikisho hilo Gianni Infantino uliidhinishwa kwa kauli moja na wanachama wa Fifa mjini Zurich Jumanne.
BBC
No comments:
Post a Comment