Unaweza ukaona safari ya kutoka Mwanza
mpaka Dar es Salaam ni ndefu kwa sababu unatumia kati ya saa 12 mpaka 16
ndani ya basi, lakini kwa Usafiri wa Ndege ni kama saa moja tu hivi
unakuwa umemaliza safari !!
Sasa hizo saa za kukaa kwenye basi safari ya Mwanza-Dar
kuna watu wanazitumia wakiwa angani kwenye Ndege… Nimezipata Rekodi
Mitandaoni, zinaonesha safari kumi za Ndege ambazo wasafiri wanatumia
muda mwingi zaidi hewani kwenye safari moja.
1.Dubai Mpaka Panama– Hii ni Safari ambayo inachukua
saa 17 na dakika 35 angani… yani Ndege ikiruka Dubai hakuna sehemu
inatua mpaka ifike Panama. Hii ndio safari ndefu zaidi kwa sasa ambayo
inafanywa na Ndege za
Emirates… umbali toka
Dubai mpaka
Panama ni Kilometa 13, 820.
2. Dallas mpaka Sydney- Unaambiwa umbali toka
Dallas Marekani mpaka
Sydney Australia ni Kilometa 13,804. Hiyo ni safari ambayo inachukua saa 17 kwa Ndege za
Qantas.
3. Atlanta mpaka Johannesburg–
Hapo kuna umbali wa Kilometa 13,580.. safari hii inakamilika kwa Ndege
za Shirika la Delta kukaa angani kwa saa 16 na Dakika 55 ambazo ni kama
saa 17 hivi mwanzo mpaka mwisho wa safari.
4. Los Angeles mpaka Dubai–
Kama kuna wakati unawaza kufanya safari kati ya hayo Majiji mawili,
basi utambue kabisa kwamba umbali wake ni Kilometa 13,420.. na Ndege
inatumia saa 16 na Dakika 30. Hii sio safari fupi hata kidogo mtu wangu
!!
5. Los Angeles mpaka Jeddah– Shirika la Ndege la Saudi Arabia ndio ambao wamekamata hii njia, unaambiwa umbali toka Los Angeles Marekani mpaka Jeddah Saudi Arabia inakuchukua saa 17 pia kuimaliza hiyo safari yenye umbali wa Kilometa 13,409.
Picha ya muonekano wa juu wa Jeddah Airport mpya, Saudi Arabia.
6. Los Angeles mpaka Abu Dhabi–
Umbali kati ya hiyo Miji miwili ni Kilometa 13,500.. sio safari ndogo
aisee, Ndege za Etihad zinakamilisha hiyo safari kwa saa 16 na Dakika 50
mwanzo mwisho.
7. Houston mpaka Dubai–
Kilometa 13,145 zimetajwa kwamba ndio umbali kati ya Miji hiyo miwili,
safari yake mwanzo mpaka mwisho kwa Ndege inachukua muda wa saa 16 na
Dakika 10… Ndege za Emirates zinahusika pia kusafirisha watu kati ya Miji hii miwili.
8. San Francisco mpaka Abu Dhabi– Umbali kati ya hiyo Miji ni Kilometa 13,130.. na safari yake inachukua saa 16 kukamilika.
9. Dallas mpaka Hong Kong–
Hapo unazungumzia Marekani na China, umbali wake ni Kilometa 13,700 na
umbali huo kwa safari ya Ndege inachukua saa 16 na Dakika 15… Ndege za American Airlines zimeunganisha hii Miji miwili kwa Ndege za moja kwa moja.
10. San Francisco mpaka Dubai– Hii nayo imo kwenye list ya safari ndefu za Ndege, umbali wake ni Kilometa 13,040… Ndege za Emirates zimeunganisha hii Miji pia kwa safari ya Ndege ya moja kwa moja. Safari yote inakamilika ndani ya saa 16 na Dakika 40.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog