Friday, September 25, 2015

WATAKA MAGEUZI VIPINDI VYA HIJJA

Maafa Mecca: Mfalme ataka mageuzi hijja

Mfalme Salman wa Saudi Arabia ametoa agizo la kupitiwa upya kwa masuala ya Hijja baada ya watu zaidi mia saba kufariki kutokana msongamano Minna  Macca.
Watu wengine mia nane walijeruhiwa katika tukio hilo.Vifo hivyo ni vingi kutokea katika Hijja kwa takriban miaka ishirini na tano iliyopita.
Maafa hayo yalitokea mahujaji takriban milioni mbili walipokuwa wakishiriki moja ya Ibada  muhimu za mwisho.
Ndio mkasa mbaya zaidi kutokea wakati wa Hijja katika kipindi cha miaka 25.
Mahujaji husafiri hadi Mina wakati wa kuhiji kurusha mawe saba kwenye nguzo saba zijulikanazo kama Jamarat, ambazo huwakilisha shetani.
Nguzo hizo zimo katika eneo ambalo inaaminika Nabii Ibrahim alijaribiwa na shetani.
Watu walikuwa wakielekea eneo la kurushia mawe, na wengine wakitokea huko pale ghafla watu walipoanza kuanguka.
Kulikuwa na raia wa Nigeria, Niger, Chad na Senegal miongoni mwa mataifa mengine.
Idara ya ulinzi wa raia Saudi Arabia imesema mkanyagano huo ulitokea pale kulipotokea "ongezeko la ghafla" la watu waliokuwa wakielekea kwenye kwenye nguzo za kurushiwa mawe.
Waziri wa afya wa Saudi Arabia Khaled al-Falih amesema mkanyagano huo ulitokea kwa sababu mahujaji walikosa kufuata maagizo.
Toka kutokea maafa ya Winchi na hili la jana watu mbalimbali kupitia blog hii wamekuwa wakiuliza kuhusu msanii wa maigizo Afrika Mashariki, Mzee Majuto.
Kufuatia kupata nafasi kwenda Hijja Mzee Majuto amekuwa akileta simulizi nyingi na watu kutaka kujua ima kwa hali moja au nyengine.
Ila ukweli ni kuwa Mjuto ni Bukheri wa Afya na asubuhi hii alizungumza na tangakumekuchablog na kusema ni mzima na kuwataka Watanzania kumuombea Dua kwa Mwenyezi Mungu arejee salama.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment