Tuesday, September 22, 2015

MAZIWA 10 YENYE MUONEKANO MFUMO WA MOYO

Du!! Tazama maziwa 10 yanayotajwa kuwa na muonekano wa moyo duniani ..(+Pichaz)

Huenda umewahi kutembelea vivutio vingi vya utalii duniani lakini huenda hukuwahi kubahatika kufika wala kusikia kuhusu  maziwa haya mazuri ya kuvutia yenye muonekano wa umbo la moyo au kopa. Hii ni stori ambayo nimekutana nayo mtandaoni mtu wangu wa nguvu, hivyo nikaona sio vibaya September 22 nikakusogezea karibu yako Top 10 ya maziwa yenye muonekano wa moyo duniani. Chanzo cha hii stori ni World – World Top Top. Huu ni muonekano wake kwa juu
1- Ziwa Shimshal – Pakistan
heart_shaped_shimshal_lake_pakistan (1)
Hili ni ziwa lenye umbo la moyo na lipo katika bonde la Hunza Pakistan
2- Gaislacher See – Austria
gaislacher-see-lake
Hili lipo Australia katika mlima Gaislachkogel
3- Heart Lake – Canada
heart_lake_ompah_canada
Hili lipo Canada pembeni limezunguukwa na maua mazuri lipo karibu na Ompah, Ontario
4- The Coeur de Voh – New Caledonia
heart_shaped_coeur_de_voh_new_caledonia
Muonekano wake kwa juu umepambwa na maua yanayoelea juu ya maji.
5- Crater – Uturuki
heart_shaped_narlıgöl_lake_turkey
Crater lipo Uturuki mpakani mwa Cappadocia
6- Heart Lake – Urusi
heart_lake_peak_cherkogo_russia
Lipo Urusi na inatajwa kama unataka kuona muonekano wake kwa juu utatumia masaa 5 kupanda kilele cha mlima Cherskogo
7- Hili ni bwawa lipo USA (Marekani)
heart_shaped_lake_ohio
Bwawa hili pia lipo karibu na Strongsville Ohio
8- Chicago – Colorado – USA
chicago_lakes_mt_evans_colorado
Sio lazima ulitazame kwa juu ili ujue kama lina umbo la moyo hata kwa chini ukitazama Chicago linaonekana kuwa na umbo hilo.
9- Aral Sea – Kazakhstan
heart_shaped_aral_sea
Sehemu ya Kusini ya Aral Sea ndio inaonyesha muonekano wa umbo la moyo
10- Eros  – India
heart_shaped_eros_lake_chembra
Ukiwa unaelekea kilele cha mlima Chembra ni rahisi kuona muoneka wa Eros.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment