Wachina na rekodi za nguvu, safari hii wana hili Daraja lililotengenezwa kwa kioo juu ya Milima ..!!
Kutokana na ukuaji wa Teknolojia pamoja
na kasi kubwa iliyopo Duniani kwenye soko la Ushindani na Ubunifu, kila
siku tunaona ubunifu mkubwa sana ukigusa headlines za habari kubwa
Duniani !!
Kulikuwa na magari yanayotumia mafuta,
zimekuja gari zinazotumia na nishati nyingine ikiwemo gari za umeme..
ikaja stori kwamba badala ya kupokeza muda kuchaji gari, Uingereza
wakaitambulisha teknolojia ya barabara zinazochaji gari za umeme… hiyo
ni mfano tu wa stori za kukua kwa teknolojia kwenye kasi kubwa sana
Duniani.
Ninalo Daraja la kioo toka China… Daraja
limekamilika na lina urefu wa kama Mita 300 hivi ambazo kwa hesabu ya
kawaida ni urefu wa viwanja vitatu vya mpira, yani kutoka goli mpaka
goli alafu viwanja viwe vitatu !!
Unaambiwa kwamba upana wa kioo
kilichotumika kwenye huu ujenzi kina kama Milimita 24 ambazo ni kama
mara 25 ya upana wa kioo cha kawaida, kwa hiyo hakuna shaka kuhusu
uimara na usalama wa Daraja lenyewe !!
Daraja hilo limejengwa kuunganisha sehemu ambayo ni juu ya Milima kwenye Hifadhi ya Shiniuzhai Park, ambayo iko kwenye Jimbo la Hunan, Kusini mwa China.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment