Bei ya dawa ya ukimwi yapandishwa 5000%
Kampuni moja ya
kutengeza madawa imelazimika kujitetea vikali baada ya kupandisha
gharama ya dawa ya Ukimwi kwa asilimia 5,000%.
Hii inamaanisha kuwa bei ya tembe moja ya dawa inayotumika kupunguza makali ya ukimwi itapanda kutoka dola $13.50 hadi $750.Kampuni hiyo inayoitwa Turing Pharmaceuticals imelaumiwa na Wadau wa maswala ya Ukimwi kwa kuongeza bei ya dawa hiyo ya Daraprim ambayo imekuwa mstari wa mbele katika kuimarisha uwezo wa mwili wa mgonjwa aliyeathirika kupigana na maambukizi mapya.
Daraprim inauzwa kwa bei nafuu zaidi ikilinganishwa na dawa zinazotibu magonjwa sawa.
Shkreli aliiambia runinga ya Bloomberg katika mahojiano ya kibinafsi.
Daktari Wendy Armstrong kutoka muungano wa wauguzi nchini Marekani HIV Medicine Association amelaumu sababu zilizotolewa kwaajili ya nyongeza hiyo kubwa ya bei ya dawa hiyo.
Rais wa chama cha Democratic Hillary Clinton ameonya kuwa Serikali yake itachukua hatua kali dhidi ya makampuni yanayofaidi kutokana na msiba wa watu kwa kupandisha bei ya madawa maalum.
Chanzo BBC
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment