Tangakumekuchablog
Tanga,JESHI la
Polisi Mkoani Tanga limesema limejipanga kuhakikisha wananchi
wanasherehekea Sikukuu ya Idd El Hajj kwa amani na utulivu na kutoa ovyo kwa
madereva wa vyombo vya moto kuzingatia sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari,
ofisini kwake jioni hii, Kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Zuberi Mombeji, alisema polisi
itazidisha doria siku zote za Sikukuu kwa kutumia askari wa miguu wanaotumia
mbwa na farassi pamoja na wa pikipiki.
Alisema itafanya doria katika maeneo
ambayo ni korofi yanayotambulika kwa uporaji na wizi hivyo kuwahakikishia
wananchi kuondoa hofu na kuwataka wazazi kuwa makini na watoto wao wakati wa
matembezi.
“Sisi polisi niseme kuwa tumejipanga
vilivyo na kuwahakikishia wananchi kusherehekea Idd kwa amani na
utulivu----tuko na vikosi vya askari wanaotumia mbwa na farasi na wale wa
pikipiki kazi yao ni kupita chochoroni kwa doria” alisema Mombeji na kuongeza
“Lakini niwaase marafiki zangu wa
bodaboda kuwa mimi mwenyewe nitaongoza usalama barabarani ----bodaboda yeyote
au dereva wa gari ataevunja sheria sikukuu ataililia korokoroni” alisema
Aliwataka madereva hao kuepuka
kutumia vilevi na kuendesha vyombo vyao jambo ambalo amesema hatumvumilia mtu
yoyote na sheria itatumika bila huruma na hivyo kuwaasa kuwa makini.
Kwa upande wa wazazi, kamanda
Mombeji aliwataka kuwapa watoto wao wakati wa matembezi watu wenye uelewa ikiwa lengo ni kuepuka
kupotea pamoja na usalama wakati wakiwa katika matembezi barabarani.
Alisema vipindi vya sikukuu
hujitokeza upotevu wa watoto jambo ambalo linasababishwa na wazazi kuwaruhusu
watoto wao kufuatana na watu ambao hawajitambui.
Alisema jambo hilo limekuwa kero na
kusababisha vipindio hivyo vya sikukuu wazazi na walezi kujazana katika vituo
vya polisi kulizia watoto wao na hivyo kutaka lisijitokeze tena.
“Niwaombe wazazi kwanza kuwa makini
na nyumba zao kwani wadokozi huutumia mwanya huo kwa kufanya udokozi----na
ikumbukwe kuwaruhusu watoto wenu kwa kuongozana na watu wenye kujitambua”
alisema Mombeji
Akitoa mkono wake wa Idd kwa wakazi
wa Tanga, kamanda aliwatakia Sikukuu ya furaha na amani na kusema kuwa furaha
hiyo iwe mwanzo mzuri wa kuelekea uchaguzi mkuu usikuwa na matukio ya uvunjifu
wa amani.
Mwisho
No comments:
Post a Comment