Sunday, September 20, 2015

WENGI WAMLAUMU REFA WA MCHEZO WA ARSENA NA CHELSEA

WENGER, FERDINAND, WAMSHAMBULIA DIEGO COSTA

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amechukizwa na tabia za mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa ambaye aliwachezea rafu walinzi wa Arsenal huku akimuingiza beki Gabriel Paulista wa Arsenal katika mtego wa kadi nyekundu.
Wenger amemponda mwamuzi Mike Dean kwa kile alichosema alimuogopa Diego Costa ambaye alistahili kupewa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya mlinzi mwingine wa Arsenal Laurent Koscienly lakini Mike Dean akaishia kumpa kadi ya njano.
Wenger pamoja na wachambuzi wengi wa soka nchini England wamemshangaa Mike Dean kwa kushindwa kumtoa nje Costa kwa kuwa chanzo cha yote yaliyotokea, huku Rio Ferdinand akimtaja Costa kuwa amekosa ueledi.
Alan Shearer amemlaumu Paulista kwa kuingia katika mtego wa tabia za Diego Costa na kusababisha kutolewa nje kwa kadi nyekundu. Katika mechi hiyo ambayo Arsenal walifungwa mabao 2-0 iliisha kwa Arsenal kuwa pungufu ya wachezaji wawili mara baada ya Saint Carzola nae kuoneshwa kadi nyekundu.
Watu wengi nchini England wanataka kuona FA ikichukua hatua dhidi ya Diego Costa ikiwa ni pamoja na kumfungia pamoja na  kwa tabia zake za kuwatupia makonde wapinzani pamoja na mchezo wake usio wa  kistaarabu.
Kwa habari, matukio na michezo ni jhapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment