Zinazotajwa kuwa sababu za Arsenal kuwakosa Edinson Cavani, Karim Benzema na Lewandowski zipo hapa
Klabu ya soka ya Arsenal
ilikuwa ikihusishwa kutaka kuwasajili wachezaji kadhaa katika dirisha
la usajili lililofungwa mwezi August lakini haikufanikiwa na hatimaye
ilifanikiwa kumsajili kipa wa zamani wa Chelsea Peter Cech kwa dau la pound milioni 10, miongoni mwa majina yaliyokuwa yakitajwa kutaka kusajiliwa na Arsenal ni Karim Benzema, Edinson Cavani na Robert Lewandowski.
September 24 stori kutoka mtandao wa express.co.uk umeandika chanzo cha Arsenal kuwakosa nyota hao, licha ya Robert Lewandowski kutopewa kipaumbele katika klabu yake ya FC Bayern Munich chini ya kocha Pep Guardiola, wakala wa mchezaji huyo Cezary Kucharski alithibitisha kuwa Lewandowski haipendi hali ya hewa ya Uingereza.
Karim Benzema alikuwa ni mmoja kati ya mastaa wa soka waliokuwa wakisakwa na Arsenal katika kipindi cha usajili cha mwezi August, kwani alikuwa akihusishwa kujiunga na Arsenal kwa dau la poundi milioni 40. Lakini nguli wa zamani wa klabu ya Arsenal Ian Wright alilaumu mipango ya Arsenal kwani kilichofanya Arsenal wamkose Benzema ni kutokwenda kufanya mazungumzo ya awali na mchezaji kwani kufanya hivyo Ian Wright ana amini ingesaidia. Ila amekiri kuumizwa na tweet ya Benzema ya kusema Real Madrid ni nyumbani.
Kwa upande wa Edinson Cavani licha ya picha ya yeye akiwa pamoja na kocha wa Arsenal Arsene Wenger kuvuja wakiwa Ufaransa, alinukuliwa kukiri kuhitajika na Wenger katika baadhi ya magazeti ya Ufaransa lakini amekuwa akiuhusishwa kujiunga na vilabu kadhaa katika dirisha la usajili la mwezi August lakini PSG ni mahali sahihi kwake na bado wanamuamini.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment