Baada ya msimu mbovu Liverpool Balotelli kafunga goli umbali wa mita 27..
Baada ya kuwa na msimu mbovu katika klabu ya Liverpool uliyopelekea kutoitwa katika timu yake ya taifa ya Italia Mario Balotelli ameanza kurudi katika ubora wake baada ya kufunga moja kati ya magoli mazuri ya faulo katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Udenise.
Mario Balotelli
alipachika goli hilo dakika ya tano ya mchezo baada ya kupiga faulo
kutoka umbali mita 27 na kuingia wavuni moja kwa moja, hili ni goli la
kwanza kwa mshambuliaji huyo wa kiitaliano aliyeshindwa kufanya vizuri
katika klabu ya Liverpool ya Uingereza na kujiunga kwa mkopo wa muda mrefu katika klabu yake ya zamani ya AC Milan.
Balotelli alijiunga na klabu ya AC Milan ya Italia akitokea Liverpool katika dirisha la usajili la mwezi August kwa mkopo wa muda mrefu, Liverpool ililazimika kumtoa kwa mkopo Balotelli baada ya kushindwa kufanya vizuri katika kikosi chao, kwani hadi anaondoka Liverpool Balotelli alicheza mechi 16 na kufunga goli moja pekee.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment