Thursday, September 24, 2015

SWALA YA IDD EL HAJJ, TANGA

 Waumini wa dini ya Kiislamu jijini Tanga wakiswali Swala ya Idd El Hajj iliyoswaliwa Tangamano  leo.
Tukio la waumini wa Dini hiyo ya Kiislamu kuswali siku moja imepokelewa kwa shauku kubwa tofauti na baadhi ya miaka mengine ambapo waumini hao hutofautiana kulingana na muandamo wa mwenzi hivyo Waislamu wengi kutatizika na kushindwa kufuata upande upi ambao kwa namna mmoja au nyengine ni sahihi.
Baadhi ya waumini wamezunguma na tangakumekuchablog na kusema kuwa huo ni mwanzo mzuri na kuwataka Masheikh kuwa na Shura ya mara kwa mara hasa karibu na vipindi vya Sikukuu ambapo hutegemea muandamo wa mwezi.
Sheikh Mohammed Abubakary wa Mwahako amesema ni tukio na furaha na faraja Waislamu Duniani kote kuswali Idd Siku moja hasa Sikukuu ya Idd El Hajj ambayo ni nadra sana kuswali siku moja.
Amesema Sikukuu ya Idd El Fitri hutokea waumini kuswali siku moja na kutofautiana kwa baadhi ya miaka lakini kudai kuwa hii ya Idd El Hajj ni tukio la Historia.





No comments:

Post a Comment