Mamia wafariki katika mkanyagano Mecca
Watu zaidi ya 717
waliokuwa wakishiriki sherehe za Hijja wamefariki kwenye mkanyagano
uliotokea karibu na mji mtakatifu wa Kiislamu wa Mecca, maafisa nchini
Saudi Arabia wamesema.
Idara ya ulinzi wa raia nchini humo imesema
watu wengine 863 wamejeruhiwa katika kisa hicho kilichotokea eneo la
Mina, takriban kilomita tano kutoka mji wa Mecca.Maafa hayo yalitokea mahujaji takriban milioni mbili walipokuwa wakishiriki moja ya kaida muhimu za mwisho katika ibada za hija.
Ndio mkasa mbaya zaidi kutokea wakati wa Hijja katika kipindi cha miaka 25.
Mahujaji husafiri hadi Mina wakati wa kuhiji kurusha mawe saba kwenye nguzo saba zijulikanazo kama Jamarat, ambazo huwakilisha shetani.
Nguzo hizo zimo katika eneo ambalo inaaminika Nabii Ibrahim alijaribiwa na shetani.
Watu walikuwa wakielekea eneo la kurushia mawe, na wengine wakitokea huko pale ghafla watu walipoanza kuanguka.
Kulikuwa na raia wa Nigeria, Niger, Chad na Senegal miongoni mwa mataifa mengine.
Idara ya ulinzi wa raia Saudi Arabia imesema mkanyagano huo ulitokea pale kulipotokea "ongezeko la ghafla" la watu waliokuwa wakielekea kwenye kwenye nguzo za kurushiwa mawe.
Chanzo BBC
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment