Tuesday, September 29, 2015

VICTOR VALDES, KUFUNGASHIWA VIRAGO VYAKE OLD TRAFORD

Klabu ya Manchester United ipo tayari kuvunja mkataba na golikipa wa kihispania Victor Valdes, baada ya pande zote mbili kukaa chini na kukubaliana kuhusiana na suala hilo, Klabu ya Manchester United ipo tayari kumuachia golikipa huyo ila kama atakubali kuhamia timu ya nje ya Uingereza.
victor-valdes-manchester-united-u21s_3256808
Huu umekuwa ni utamaduni wa vilabu vingi duniani hususani vilabu vya Uingereza havipendi kuuza mchezaji katika klabu pinzani, kwani wengi wamekuwa wakiamini kumuuza mchezaji ndani ya klabu inayoshiriki Ligi Kuu Uingereza ni sawa na kumuuzia adui yako silaha.
Victor-Valdes-Man-Utd-Debut
Mkataba wa Victor Valdes na Manchester United unamalizika mwishoni mwa msimu huu, ila kurejea kwa David de Gea katika kikosi cha kwanza kunatoa nafasi ya Valdes kuondoka, sababu za Valdes kupewa nafasi ya kuhama klabu hiyo zinatokana na kugombana na kocha wa Man United Louis van Gaal, klabu ya Man United haipendi kuona akijiunga na timu inayoshiriki Ligi Kuu Uingereza hususani timu zilizo nafasi nne za juu.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment