Monday, September 21, 2015

ETHIOPIA WAMEANZA MATUMIZI YA TRENI ZA UMEME

Ethiopia wameanza rasmi kutumia Treni za abiria zinazotumia umeme.



ET 3Ripoti inasema Treni hizi ambazo zimezinduliwa September 20 2015 zinaanza kubeba abiria na zinatarajiwa kurahisisha usafirishaji wa watu kwenye mji mkuu wa Addis Ababa, Ethiopia nchi ambayo mpaka mwaka huu wanasema idadi ya watu wake ni zaidi ya MILIONI 90.
ET 2BBC wanasema hizi Treni zimetajwa kuwa mfano na za kwanza kusini mwa jangwa la sahara ambapo ujenzi na uendeshaji wa huduma hii ya reli unatekelezwa kwa ushirikiano na serikali ya China.
ET 4
ETPicha zote ni kutoka BBC.
ET 6Treni hizi za umeme zitakua na uwezo wa kuhudumia Abiria elfu kumi na tano ndani ya dakika 60 ambapo Treni moja inaweza kubeba abiria 286 kwa wakati mmoja.
ET 5Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment