Monday, September 28, 2015

RAIS MALDIVES ANUSURIKA KIFO

Rais wa Maldives anusurika mlipukoMaldives

 

Rais wa Maldives Yameen Abdul Gayoom , amenusurika katiko mlipuko uliotokea kwenye boti yake alipokuwa akirejea nchini humo baada ya kuhiji Saudi Arabia.
Waziri Mohamed Shareef amesema mlipuko huo umetokea katika  boti hiyo ya mwendo wa kasi ilipokuwa ikiingia eneo la kuegesha boti katika mji mkuu Male.
Mke wa Rais  Fathimath Ibrahim na mmoja wa msaidizi wake wamepata majeraha madogo, amesema. Hata hivyo mlinzi mmoja amepata majeraha mabaya.
Shareef amesema chanzo cha mlipuko huo, unaodaiwa kuanza eneo la injini la boti hiyo, bato hakijabainika.
Chanzo BBC
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablo

No comments:

Post a Comment