Wednesday, September 30, 2015

COASTL UNION YATANDIKWA BILA HURUMA NA WASAGAJI UNGA


AZAM FC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. 
Mchezo huo uliocheeshwa na refa Alex Mahagi wa Mwanza, mabao ya Azam yalifungwa na beki Shomary Salum Kapombe na mshambuliaji Kipre Herman Tchetche raia wa Ivory Coast, yote kipindi cha pili.
Kipre Tchetche ameendela kuifungia Azam FC Ligi Kuu 

Kapombe alifunga bao safi dakika ya 47 akimalizia mpira wa kona uliopigwa na winga Farid Mussa, wakati Kipre Tchetche alifunga dakika ya 74 akimalizia krosi ya kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy.’
Refa Mahagi alimtoa nje Kocha wa Azam FC, Muingera Stewart Hall baada ya kupishana kauli na mwamuzi wa kiba dakika ya 79.
Azam FC inatimiza pointi 15 baada ya kushinda mechi zake zote tano za mwanzo za Ligi Kuu.
Kikois cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Racine Diouf, Pascal Wawa, Said Mourad, Farid Mussa, Frank Domayo, Jean Baptiste Mugiraneza, Ramadhani Singano ‘Messi’/Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dk65, Allan Wanga/Didier Kavumbangu dk72 na Kipre Tchetche/Ame Ali ‘Zungu’ dk77.
Coastal Union; Sebwato Nicholas, Hamad Juma, Tumba Lui, Yassin Mustafa, Abdallah Mfuko, Youssoufa Sabo, Twaha Ibrahim ‘Messi’, Nassor Kapama/Mohammed Hamisi dk56, Ali Ahmed ‘Shiboli’/Chidiebele Abasalim dk61, Ayoub Yahaya na Ismail Mohammed.

No comments:

Post a Comment