Tuesday, September 22, 2015

FA YAZISHITAKI ARSANAL NA CHELSEA

Diego Costa na Gabriel washtakiwa na FA

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa ameshtakiwa kwa madai ya kutaka kuzua ghasia ambayo hayakuonekana na maafisa wa mechi hiyo lakini ambayo yalinaswa katika ukanda wa video.
Mshambuliaji huyo alihusishwa katika kisa na beki wa Arsenal Laurent Koscielny katika dakika ya 43 ya mechi.
Mchezaji huyo ana hadi saa kumi na mbili hapo alhamisi jioni kujibu mashtaka hayo.
  Beki wa Arsenal Gabriel ameshtakiwa kwa utovu wa nidhamu kwa tabia yake wakati alipopewa kadi nyekundu huku Santi Carzola akionywa kuhusu tabia yake mbaya.
Wakati huohuo vilabu vyote viwili vimeshtakiwa kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake chini ya sheria za FA.
Vilabu vyote viwili pamoja na Gabriel  hadi saa kumi na mbili jioni siku ya Alhamis kujibu mashtaka hayo.
Kwa habario, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment