Tuesday, September 29, 2015

UZEMBE WA KIPA WA ARSENAL (OSPIMA) WAIGHARIMU ARSENAL NA KUDUNDWA BAO 3, 2



MATOKEO YA LIGI YA MABINGWA ULAYA
Septemba 29, 2015  
Maccabi Tel Aviv 0-2 Dynamo Kyiv 
FC Porto 2-1 Chelsea 
Barcelona 2-1 Bayer 04 Leverkusen 
BATE Borisov 3-2 Roma
Arsenal 2-3 Olympiakos
Bayern Munich 5-0 Dinamo Zagreb
Zenit St Petersburg 2-1 KAA Gent
Lyon 0-1 Valencia CF
Mechi za Leo Jumatano Septemba 30, 2015
FC Astana v Galatasaray
CSKA Moscow Vs PSV 
Juventus Vs Sevilla
Borussia Monchengladbach Vs Manchester City
Malmo FF Vs Real Madrid
Manchester United Vs VfL Wolfsburg
Atletico MadridVs Benfica
Shakhtar Donetsk Vs Paris Saint-Germain
Luis Suarez akishangilia baada ya kuifungia bao la ushindi Barcelona dakika za mwishoni dhidi ya Bayer Leverkusen

MABINGWA watetezi, Barcelona wamepata ushindi mwembamba wa mabao 2-1 usiku huu katika mchezo wa Kundi E Ligi ya Mabingwa Ulaya, dhidi ya Bayer 04 Leverkusen ya Ujerumani Uwanja wa Camp Nou.
Katika mchezo huo, ambao wenyeji walianza kuikosa huduma ya Mwanasoka Bora wa Ulaya, Lionel Messi ambaye ni majeruhi, wageni walitangulia kupata bao kupitia kwa Kyriakos Papadopoulos dakika ya 22.
Hata hivyo, Sergi Roberto Carnicer aliisawazishia Barca dakika ya 80 kabla ya Luis Suarez kufunga la pili dakika mbili baadaye.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, BATE Borisov imeshinda 3-2 nyumbani dhidi ya Roma, mabao yake yakifungwa na Igor Stasevich na Filip Mladenovic mawili, wakati ya wapinzani wao yamefungwa na Gervais Kouassi na Vasilis Torosidis.



Mshambuliaji wa Bayern Munich, Robert Lewandowski ameendelea kutisha kwa mabao baada ya kufunga hat-trick

Bayern Munich imeshinda 5-0 dhidi ya Dinamo Zagreb mchezo wa Kundi F, Uwanja wa Allianz Arena mabao yake yakifungwa na Douglas Costa de Souza dakika ya 13, Robert Lewandowski matatu dakika za 21, 28 na 55 na Mario Gotze dakika ya 25.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, Arsenal imefungwa mabao 3-2 nyumbani Uwanja wa Emirates na Olympiakos. Mabao ya The Gunners yamefungwa na Theo Walcott dakika ya 35 na Alexis Sanchez dakika ya 65, wakati ya Olympiakos yamefungwa na Felipe Pardo dakika ya 33, David Ospina aliyejifunga dakika ya 40 na Alfred Finnbogason dakika ya 66.
Chelsea imechapwa mabao 2-1 ugenini na FC Porto katika mchezo wa Kundi G Uwanja wa. Mabao ya Porto yamefungwa na Andre Filipe Bras Andre dakika ya 39 na Maicon Pereira Roque dakika ya 52, wakati bao pekee la The Blues limefungwa na Willian Borges Da Silva dakika ya 47.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, Maccabi Tel Aviv imefungwa 2-0 nyumbani na Dynamo Kyiv, mabao ya Andriy Yarmolenko na Aluisio Chaves Ribeiro Moraes Junior Uwanja wa Bloomfield.
Cesc Fabregas (kulia) na Diego Costa (katikati) wakiwa taabani baada ya kipigo. Kushoto ni Maicon
Zenit St Petersburg imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KAA Gent katika mchezo wa Kundi H mabao yake yakifungwa na Artem Dzyuba dakika ya 35 na Oleg Shatov dakika ya 67, wakati bao la wageni limefungwa na Thomas Matton dakika ya 56 Uwanja wa Petrovski.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, Valencia ya Hispania imeshinda ugenini 1-0 dhidi ya Lyon ya Ufaransa bao pekee la Sofiane Feghouli dakika ya 42 Uwanja wa Stade de Gerland. 
David Ospina akisikitika baada ya kuwaruhusu Olympiakos kupata bao

Michuano hiyo itaendelea leo n Jumatano, FC Astana ikiikaribisha Galatasaray Uwanja wa Astana Arena, CSKA Moscow ikiikaribisha PSV Uwanja wa Arena Khimki, Juventus ikiikaribisha Sevilla Uwanja wa Juve, Borussia Monchengladbach ikiwakaribisha Manchester City Uwanja wa Borussia-Park, Malmo FF ikiwakaribisha Real Madrid Uwanja wa Swedbank, Manchester United ikiwakaribisha VfL Wolfsburg Uwanja wa Old Trafford , Atletico de Madrid ikiwakaribisha Benfica Uwanja wa Vicente Calderon na Shakhtar Donetsk wakiwakaribisha Paris Saint-Germain Uwanja wa Lviv. 

No comments:

Post a Comment