Friday, September 25, 2015

KISIWA KITEMBEACHO KATIKA MAJI KAMA BOTI, KIKO HAPA

Umewahi kuona kisiwa kinahama? Hiki hapa, unaweza kuhisi ni Boti au Meli ..!!

Ubunifu wa binadamu na maendeleo ya Teknolojia ni vitu ambavyo huwa vinatuletea mambo mapya kila siku, hakuna mtu asiyependa kusifiwa baada ya kufanya kazi nzuri.. ubunifu wa hiki kisiwa ni kazi nzuri ambayo tayari pongezi zimeanza kuwafikiwa wabunifu walioona kuna umuhimu kuwa na kitu kama hiki cha kuvutia.
Tunajivunia uzuri wa Zanzibar yetu, huo ni uzuri kwenye kisiwa cha asili kabisa.. taarifa ikufikie kwamba wapo waliowaza kutengeneza kisiwa kinachohama kwa kutembea juu ya maji kama ilivyo meli au Boti.
Najua kwamba Dunia inavitambua pia visiwa vilivyotengenezwa na binadamu ikiwepo Palm Island, ambacho kiko Dubai… lakini Dunia inatambulishwa pia kwenye Kisiwa ambacho kimebuniwa na wataalam wa Kampuni ya Migaloo ambao wanadili sana na kutengeneza Boti za kifahari.
150918124529-migaloo-floating-island-overview--super-169
Muonekano wa juu wa Kokomo Ailand, kisiwa cha aina yake ambacho kinatembea juu ya maji.
Ubunifu huu utasogezwa kwenye Maonesho maalum ya Monaco Yatch Show na tayari watu wenye pesa zao wameonekana kuvutiwa sana na hii kitu, kwa hiyo tayari ni biashara ambayo inatarajia wateja wa nguvu kabisa any time kuanzia sasahivi !!
150918125750-migaloo-floating-island-city-super-169
Ukiangalia nje mpaka ndani Kisiwa hiki kinavutia, na kina mahitaji yote muhimu kwa mtu anayehitaji kuishi ndani yake, kwenye vilivyomo unaambiwa mpaka Beach za nguvu kabisa zipo ndani !!
tumblr_inline_nv6lgtcn8I1tvnn6i_500
150918125046-migaloo-floating-island-interior-super-169
Ndani kunavutia mtu wangu, yani huku ndani unaambiwa kuna Beach nyingine na mazingira poa kabisa ya kujienjoy !! Ukiingia mpaka unajisahau kwamba uko kwenye kisiwa kinachoelea.
  150924122848-kokomo-ailand-top-view-super-169
Ubunifu huo wa teknolojia ina mazuri yake ya kuvutia kila siku yani !!

Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment