Wednesday, September 30, 2015

AFRICAN SPOTRS BADO UGENI UNAWASUMBUA

 Mchezaji wa timu ya African Sports, Victor Agai, akiwatoka mabeki wa timu ya Mgambo JKT katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara LEO Uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga.

 , Washabiki wa timu ya African Sports wakiishangilia timu yao  wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uwanja wa CCM Mkwakwani leo.
Tangakumkekuchablog
Timu za Tanga bado hazijatulia na hivyo kuendeleza kupokea dozi ya mabao kutoka kila timu inayopambana nao na leo, African Sports imekubali kupokea kipigo cha bao 1 bila huruma  ambapo nayo Coastal Union imetandikwa mabao 2 bila huruma hivyo  na hivyo kuendeleza uteja wao
Wakati wa mchezo kuanza Sports waliuanza mpira kwa kasi na kutawala kila idara na kupelekea kukosa magoli matatu kipindi cha kwanza.
Waswahili wanasema siku ya kifo cha Nyani miti yote huteleza na ndipo wapinzani wao, Mgambo JKT ilipopata bao sekunde ya 40 tu ya mchezo kuanza.
Baadhi ya washabiki uwanjani hapo wameiambia tangakumekuchablog kuwa Sports inapaswa kujilaumu kufuatia mabao ya wazi iliyokosa.
Walisema mchezo huo ulikuwa wao baada ya kutawala kuanzia kipindi cha kwanza hadi mpira kuisha.

No comments:

Post a Comment