Monday, September 21, 2015

MGOMO SHULENI KENYA

Shule zafungwa Kenya kutokana na mgomo

Mgomo wa walimu
Wanafunzi wengi Kenya wamelazimika kusalia nyumbani baada ya kile kilichodaiwa kuwa Serikali kuagiza kufungwa kwa shule zote za umma na za kibinafsi leo kutokana na mgomo wa walimu.
Ingawa shule za umma zimefungwa, baadhi ya shule za kibinafsi zimekaidi agizo la Serikali na kuendelea na masomo.
Chama cha shule za kibinafsi kimesema kitawasilisha kesi mahakamani leo kupinga agizo hilo la Serikali lililotolewa na Waziri wa Elimu Jacob Kaimenyi Ijumaa wiki iliyopita.
Wazazi wanaowapeleka watoto wao katika shule za kibinafsi, nyingi ambazo hutoza karo ya juu, wametoa hisia kali kutokana na tangazo hilo wakishangaa ni kwa nini shule hizo zinafungwa.
Katika shule za umma, ni watahiniwa wanaojiandaa kufanya mitihani ya kitaifa waliosalia shuleni.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment