Wednesday, September 23, 2015

MBABE MAYWEATHER KUPANDA ULINGONI NA MMOJA TU, KISHA KUTUNDIKA MADALUGA

Floyd Mayweather amestaafu? Kati ya hawa saba, mmoja anamsubiri Ulingoni kufunga nae hesabu..

Baada ya Pambano la Floyd Mayweather VS Andre Berto ambalo walipigana  usiku wa kuamkia September 13 2015, Mayweather aliongea kauli hii >>> ‘Nimekamilisha kila kitu, nimefanya kila kitu kwenye mchezo wangu… Umri wangu unakaribia miaka 40, hakuna nilichobakiza kwenye Ulimwengu wa Ngumi, nahitaji kutumia muda mwingi zaidi na familia yangu>> hii ilikuwa ni uthibitisho wake kwamba yeye na masuala ya Boxing ndio yamefikia mwisho !!
mayweather15
Nje ya Ulingo stori ziko nyingi sana, japo watu wengi hawakuvutiwa na Pambalo kati ya Mayweather na Berto kutokana na kupishana kwa Rekodi zao, kuna list ambayo imepangwa na Wachambuzi wa mambo wanasema Floyd Mayweather hawezi kuishia kuandika Rekodi ya kushinda mapambano 49, wanasema lazima jamaa ataongeza pambano moja ambalo akishinda atakuwa ameandika Rekodi ya kucheza Mapambano 50 na kushinda yote ndani ya kipindi cha miaka 19 ambayo amekuwa Bondia.
485148600
Hapo ni Miguel Cotto na Canelo Alvarez, ishu iko hivi.. hawa jamaa wana pambano November 21 2015 Las Vegas Marekani, mshindi kati yao huenda akakutana na Mayweather kwenye Pambano linalofatia. Cotto ni Bondia anayesimamiwa na Kampuni ya Jay Z, Roc Nation Sports.
usa-today-8551827
Emmanuel “Manny” Dapidran Pacquiao, Bondia Mfilipino ambae alisafiri kwenda Marekani na akapigwa na Mayweather… macho ya wengi ni kuona marudio ya Pambano hilo ambalo lilivunja Rekodi kuwa na mauzo makubwa ya Ticket, Pacquiao kaingia pia kwenye list ya wanaotarajiwa kupambana na jamaa kwenye Pambano lijalo.
garcia_1719752a
Danny Garcia, jamaa ana Rekodi nzuri pia ya kushinda Mapambano 31 na hajapigwa Pambano hata moja, kati ya Mapambano hayo.. 18 ameshinda kwa Knockouts… Nae kaingia kwenye list ya wanaosubiri maamuzi ya Mayweather kurudi tena Ulingoni.
khan_3219171
Amir Khan, Bondia wa Uingereza mwenye Rekodi ya kucheza Mapambano 31 lakini kati ya hayo alipigwa kwenye Mapambano matatu tu. Huyu nae yumo kwenye list ya Mayweather.
interim-wba-weltweight-champion-keith-thurman
Keith Thurman, jamaa nae ana rekodi ya nguvu yani.. kacheza Mapambano 26 na kashinda yote, unaambiwa kwenye Ushindi wake ana Mapambano 22 aliyoshinda kwa knockouts. Huenda ikawa Mayweather VS Thurman pia pambalo lijalo.
Kell-Brook
Kell Brook, Rekodi yake ni nzuri pia.. ana jumla ya Mapambano 35 ambayo yote kashinda, na Mapambano 24 kapata ushindi kwa knockouts.
Gennady Golovkin v Osumanu Adama
Mbabe mwingine ndio huyu mtu wangu, anaitwa Gennady Golovkin… Rekodi ya ubabe wake inadhihirishwa kwenye Mapambano 33 aliyowahi kucheza, unaambiwa ameshinda yote na kati ya hayo, Mapambano 30 kayamaliza kwa ushindi wa knockouts.
Floyd ‘Money’ Mayweather anarudi Ulingoni? swali jingine ni kwamba anarudi na nani kati ya hawa wenye Rekodi za nguvu kabisa? Atafanikiwa kuandika Rekodi ya Ushindi kwenye Pambano la 50?
floyd-mayweather_2667604b
Majibu yatapatikana soon, kama pambano hili likithibitishwa basi story huenda ikawa kubwa pamoja na promo ya nguvu ambayo inaweza kufananishwa na Rekodi ya mauzo makubwa yaliyofanyika kabla ya Pambano la May 02 2015, Floyd Mayweather VS Manny Pacquiao..
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment