Mazoezi ya kunyanyua vyuma yapelekea kifo cha kijana huyu baada ya moyo wake kupasuka…
Imekuwa kawaida kwa vijana wengi siku
hizi kupenda kunyanyua vyuma ili kujenga mwili wenye misuli mikubwa na
muonekano mzuri. Utamaduni wa kubeba vitu vizito ili kujenga mwili wenye
muonekano flani wa kuvutia unazidi kushika kasi duniani kote licha ya
vijana wengi Tanzania wameonekana kuanza kufanya mazoezi ya kubeba vyuma kwa miaka ya hivi karibuni.
Stori kutoka mtandao wa dailymail.co.uk umeripoti kifo cha Andrej Gajdos kijana
mwenye umri wa miaka 19 na urefu wa futi 7 na inch 2, amefariki baada
ya kubeba chuma na kupelekea misuli ya aorta katika moyo wake kupasuka. Andrej Gajdos alikuwa anaingia Gym mara mbili kwa siku na lengo lake lilikuwa kutengeneza mwili wake kuwa kama Dwayne Johnson.
Dr John Oxley ndio aliufanyia uchunguzi mwili wa Andrej Gajdos na kuthibitisha moyo wa Andrej Gajdos
kuwa na uzito usio wa kawaida wa gram 680 wakati binadamu wa kawaida
moyo wake unatakiwa kuwa na uzito wa gram 400 hadi gram 500, hata hivyo
uchunguzi bado umeeleza Andrej Gajdos kuwa na matatizo ya mapafu kwani njia ya kupitisha hewa katika mapafu yake imetanuka. Andrej Gajdos ni raia wa Slovakia amekutwa na umauti akiwa Tesco Uingereza.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment