Friday, September 25, 2015

MZIMU WA RUSHWA BADO UNAMUMIZA KICHWA SEPP BLATTER

Haya ndio makosa aliyokutwa nayo Rais wa FIFA, kesi yake ni mahakamani…


Zile stori za viongozi wa shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA kutuhumiwa kula rushwa na kutumia madaraka vibaya, bado zinazidi kuchukua nafasi katika vyombo vingi vya habari duniani, September 25 kutoka mtandao wa dailymail.co.uk umetangaza kuwa ofisi ya mwanasheria mkuu Uswiss imemfungulia mashitaka Rais wa FIFA Sepp Blatter.
2CC2AECE00000578-3249145-image-m-26_1443193310410
Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA Michel Platini
Taarifa kutoka ofisi ya mwanasheria mkuu inamtuhumu Blatter kwa makosa kadhaa ikiwemo ya utawala mbovu, kuingia mikataba mibovu ya haki za matangazo ya TV akiwa pamoja na aliyekuwa Rais wa mpira wa miguu wa CONCACAF  Jack Warner mwaka 2005. Blatter pia anatuhumiwa kumlipa pound milioni 1.3 kinyume na taratibu Rais wa Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) Michel Platini mwaka 2011 ikiaminika kuwa zilitumika kwa kampeni.
2CA1AFBD00000578-3249145-image-a-27_1443193328413
Rais wa zamani wa CONCACAF Jack Warner
Ofisi ya mwanasheria mkuu Uswiss imeripoti kumfungulia mashitaka Sepp Blatter September 24. Ofisi ya Rais wa FIFA Sepp Blatter imechunguzwa mchana wa September 25 mjini Zurich Uswiss kama sehemu ya kuendelea kufanya uchunguzi kwa mamlaka husika.
2CC1FBBE00000578-3249145-image-a-5_1443191725765
Hawa ndio waandishi wa habari waliokuwa wamejitokeza katika mkutano ambao Blatter alipanga kufanya lakini ulihairishwa.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment