Tangakumekuchablog
Tanga, JESHI la
Polisi Mkoani Tanga linamshikilia Mkandarasi mkazi wa Bombo Tanga, Endrew
Kimunga (54) kwa tuhuma za kusababisha ajali iliyopelekea kupinduka basi la
kampuni la Tashrif na dereva wake kufa papo hapo.
Tukio hilo lililotokea leo asubuhi
eneo la Kange nje kidogo ya jiji la Tanga baada ya dereva wa gari aina ya
Nissan Wagon, Kimunge kutoka kituo cha kuweka Petrol na kuingia barabarani
kizembe jambo lililosababisha basi la Tashrif kushindwa kulikwepa na kuingia
katika korongo na kupinduka.
Basi hilo ambalo lilikuwa likielekea
kituo kikuu cha Mabasi yaendayo Mikoani cha Kange na kuelekea Dodoma
lilipinduka baada ya dereva wake kushindwa kulikwepa jambo ambalo alilisukuma
katika korongo na kupinduka .
Akizungumza na Tangakumekuchablog,
Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Zubery Mombeji, alisema tukio hilo lilitokea
saa 12 ; 15 asubuhi eneo la Kange na kupeleka Dereva
wa basi, Mohammed Ayoub kufa papo hapo na
kusababisha majeruhi wanne.
Alisema uchunguzi wa awali
unaonyesha dereva wa Nissan Wagon, alishindwa kuzingatia sheria za barabarani
na kusababisha uzembe baada ya kuingia barabara kuu bila kuangalia magari pande
zote mbili.
“Uchunguzi wa awali unaonyesha
dereva wa gari ndogo ndie chanzo cha ajali----kwa sasa tunaendelea na uchunguzi
na tunamshikilia kwa mahojiano zaidi ya tukio zima” alisema Mombeji na kuongeza
“Dereva wa basi hakuwa na makosa ila
ni kuwa amefariki pale pale----lakini niseme kuwa bado tuko katika uchunguzi na
dereva wa Nissan tunamshikilia kituo kikuu cha Chumbageni” alisema
Aliwataja majeruhi kuwa ni Twaha Juma(42) mkazi wa Msambweni pamoja na Idd Omary ambao wote ni wafanyakazi wa kampuni ya Tashrif
Akizungumzia tukio zima la ajali
hiyo, Kamanda Mombeji, alisema Dereva wa basi hilo la Tashrif , Mohammed Ayoub,
hakufunga mkanda na kuwa chanzo cha kifo chake baada ya kurushwa mbele ya kioo
cha mbele na gari kumkokota na kupelekea kusagwasagwa.
Alisema kama angelifunga mkanda angelisalimika
kifo kama ilivyokuwa kwa wenzake wawili ambao walikuwa siti za katikati na
kupelekea kupata majeraha madogo madogo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment