Tuesday, September 29, 2015

WAFUGAJI ZIMBWABWE WABUNI VIASHRIA WAKATI NG'OMBE WAKIKATISHA BARABARA USIKU

Ng’ombe wawekwa ‘reflector’ Zimbabwe

Ng'ombe Zimbabwe
Hapa kwetu hasa katika Mikoa ya ufugaji ikiwemo Kilimanjaro na Kilindi pamoja na Handeni Mkoani Tanga kuna idadi kubwa ya wafugaji lakini hawazingatii  taratibu na sheria za mifugo na barabarani wakati wakipitisha mifugo yao.
Hili likifukuta nchini Zimbabwe wamevumbua njia ya kuzuia ajali za barabarani zinazohusisha ng’ombe wanaoranda randa.
Wamekuwa wakiwaweka kamba au vitambaa vinavyoakisi mwanga shingoni au kwenye mikia.
Wakazi hao wa wilaya ya Gutu, mkoa wa Masvingo wanasema hilo litakuwa likiwawezesha waendeshaji magari kuwatambua ng’ombe hao kutoka mbali.
Ng’ombe wengi walitoweka kwenye mashamba baada ya Wazungu wengi kufurushwa kutoka kwa mashamba yao mwaka 2000 kufuatia agizo la Rais Mugabe. Wengi wao wamekuwa wakizurura zurura bila wa kuwatunza.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment