Tuesday, September 29, 2015

WANAMGAMBO BANGUI WAVAMIA GEREZA KUWATOROSHWA WAFUNGWA

Wafungwa watoroka gerezani mjini Bangui

Mamia ya wafungwa katika Gereza moja nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati wametoroka wakati ambapo kumekuwa na machafuko yaliyosababisha watu wengi  kupoteza maisha.
Baada ya Dereva wa Taxi ambaye ni Muislamu  kuuawa, mapigano yalizuka siku ya jumamosi kati ya wanamgambo wa kikristo na makundi ya kiislamu.
Wafuasi wa wanamgambo wa kikristo wajulikanao kwa jina anti-balaka walishambulia gereza siku ya jumatatu, na kuwatorosha mamia ya Wanajeshi na wanamgambo.
Jamuhuri ya Afrika ya kati imekuwa ikikumbwa na machafuko tangu kundi la waasi wa kiislamu, Seleka kuchukua madaraka mwezi Machi mwaka 2013.
Kundi la Seleka baadae liliondolewa madarakani, hali iliyosababisha machafuko.Maelfu ya watu waliyakimbia makazi yao.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment