Saturday, September 26, 2015

CHELSEA BADO HAIJATULIA

Newcastle United Vs Chelsea matokeo ninayo hapa.


Bado mechi za Ligi Kuu Uingereza zinaendelea weekend hii, Jumamosi ya September 26 zilichezwa mechi kadhaa ila moja kati ya hiyo ni mechi kati ya Newcastle United dhidi ya Chelsea mechi ambayo ilichezwa katika uwanja wa St James’ Park, uwanja ambao una uwezo wa kuchukua zaidi ya mashabiki 50000.
Generated by IJG JPEG Library
Klabu ya soka ya Chelsea ambayo ni Bingwa mtetezi wa Ligi hiyo imeendeleza rekodi ya kutopata matokeo mazuri katika Ligi Kuu Uingereza msimu huu. Chelsea kabla ya mechi hii ilikuwa imecheza mechi 6, imeshinda 2, sare moja na kupoteza mechi 3, September 26 imenusurika kufungwa na Newcastle United katika uwanja wa ugenini.
during the Barclays Premier League match between Newcastle United and Chelsea at St James' Park on September 26, 2015 in Newcastle upon Tyne, United Kingdom.
Chelsea ambayo ipo chini ya kocha Jose Mourinho ilikubali kuruhusu goli mbili katika mchezo huo kabla ya dakika za lala salama kushituka na kuanza kusawazisha goli hizo, Mechi imemalizika kwa sare ya goli 2-2. Magoli ya Newcastle United yalifungwa na Ayoze dakika ya 42 na Georginio Wijnaldum dakika ya 60, wakati magoli ya Chelsea yalifungwa na Ramires dakika ya 79 na William dakika ya 87.
during the Barclays Premier League match between Newcastle United and Chelsea at St James' Park on September 26, 2015 in Newcastle upon Tyne, United Kingdom.
2807
Generated by IJG JPEG Library


Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment