Walinda amani wa Afrika Kusini kuadhibiwa
Wanajeshi hamsimi
wa Afrika Kusini waliokuwa wakihudumu katika kikosi cha Umoja wa Mataifa
kinacholinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Monusco)
wameagizwa kurejea nyumbani.
Viongozi wa jeshi nchini Afrika Kusini wamesema wanajeshi hao wataadhibiwa kwa kuwa wamekiuka maadili ya utendaji kazi.Taifa hilo lina takriban wanajeshi 1,400 wanaohudumu Congo, wakijaribu kusaidia kukomesha vita mashariki mwa DR Congo.
Baadhi ya wanajeshi wanadaiwa kuhatarisha usalama wa wanajeshi wengine wa UN nchini DRC Congo.
No comments:
Post a Comment