Wednesday, September 30, 2015

TASWIRA YA TANGAKUMEKUCHA LEO

  Vibarua na Nguvu kazi  katika  maduka  mtaa wa Relini Taifa road  karibu na uwanja wa Tangamano Tanga, wakiangalia mfereji ulioziba na kushindwa kupitisha maji na kusababisha takataka kujaa na kuwa  kero kwa wapita njia na wenye maduka karibu na mfereji huo.
Wanaharakati na wadau wa mazingira Tanga wamedai kuwa kukithiri uchafu na takataka katikati ya jiji la Tanga ni kutokana na watu waliopewa dhamana kutojali afya za watu.
Jiji la Tanga inadaiwa toka kupewa hadhi ya jiji yapata zaidi ya miaka 20 lakini bado sifa hiyo haiendani na mazingira halisi ya jiji hilo.
Ili kuweza kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama kwa matabaka mbalimbali ni vyema halmashauri ya jiji kuchukua hatua kali kwa wachafuzi na wale waliopewa jukumu la kuliweka jiji hilo safi kuanzia mitaro, madampo pamoja na sokoni.
Tangakumekuchablo imekuwa ikiripoti matukio ya uchafuzi na uchafu kila pembe ya jiji hilo ikiwemo mitaani, karo na chemba zinazotiririsha maji machafu pamoja na masoko na madampo yaliyojazana takataka na uchafu ikiwa na lengo la kuhakikisha jiji hilo linakuwa katika usafi na kuwa mfano wa kuigwa.
Kama mtaani kwako au uonapo kero yoyote pale usiifumbie macho, wasiliana nami kwa simu 0655 902929




No comments:

Post a Comment