Sunday, September 20, 2015

YASIKUPITE MATOKEO LIGI KUU TANZANIA BARA (VODACOM)

Wageni Ligi kuu Tanzania Bara, African Sports wana Kimanumanu bado wanachechemea na kushindwa kuhimili mikimiki ya Ligi hiyo na kuendeleza Uteja kila wanavyokutana na wapinzania wao.

MATOKEO MECHI ZA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
Jumapili Sept 20, 2015
Mwadui FC 0-1 Azam FC 
Mtibwa Sugar 2-1 Ndanda FC
Simba SC 3-1 Kagera Sugar
Coastal Union 0-0 Toto Africans
Jana Septemba 19, 2015
Stand United 2-0 African Sports
Mgambo Shooting 1-0 Majimaji FC
Prisons 1-0 Mbeya City
Yanga SC 4-1 JKT Ruvu
Nahodha John Bocco ameifungia bao pekee Azam Fc ikishinda 1-0 Mwadui

BAO pekee la Nahodha John Raphael Bocco limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Mwadui FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Huo unakuwa ushindi wa tatu mfululizo kwa Azam FC inayofundishwa na Muingereza Stewart Hall, baada ya awali kushinda 2-1 dhidi ya Prisons Uwanja wa azam Comolex, Chamazi, Dar es Salaam na 2-0 dhidi ya Stand United Uwanja Kambarage, Shinyanga.
Azam FC sasa inashuka hadi nafasi ya tatu nyuma ya Simba SC, zikiwa na pointi sawa na Yanga SC, tisa kila moja, lakini zinazidiana kwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa. 
Katika mchezo wa leo, Azam FC ilipata pigo baada ya Nahodha wake, Aggrey Morris kutolewa kwa kadi nyekundu, wakati mshambuliaji wa Mwadui FC, Rashid Mandawa alikosa penalti. 
Mechi nyingine za leo, Mtibwa Sugar imeshinda 2-1 dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro mabao yake yakifungwa na Salum Mbonde na Said Bahanuzi la wageni likifungwa na Kiggi Makassy, wakati Coastal Union imelazimishwa sare ya 0-0 na Toto Africans Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Kwa habari , matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment