Thursday, September 24, 2015

SIKUKUU YA KUCHINJA 'IDD EL HAJJ"

 Wakazi wa Donge Tanga wakichuna mbuzi ikiwa ni moja ya moja Suna kubwa ya sherehe ya Sikukuu ya Idd El Hajj iliyosherehekewa leo Duniani kote.
Uchinjaji wa mnyama iwe Mbuzi, Kondoo au Ngamia inasadikiwa kuwa ni Sunna kubwa ikiwa ni kumbukumbu ya Nabii Ibrahim pale aliposhushiwa Wahyi ya kumchinja mtoto wake na wakati alipotaka kutekeleza amri hiyo Mwenyezi Mungu alimshushia Kondoo.
Huu ulikuwa mtihani mzito wa Baba kumchinja mtoto wake kipenzi ambapo Wanavyuoni wanasema Nabii Ibrahimu alimpa mtoto huyo Ismail akiwa katia umri mkubwa hivyo alipewa mtihani huo na kuushinda.
Kwa niaba ya Uongozi na timu nzima wa Tangakumekuchablog tunatoa mkono wa Idd kwa washabiki na wapenzi wote "IDD EL MUBARKA"




No comments:

Post a Comment