Monday, September 28, 2015

NA ULEMAVU WAKE , LAKINI HAYUKO NYUMA NI MILIONEA

Huyu ndiyo mrembo mwenye ulemavu wa miguu na anaingiza Mamilioni kila siku !!

Kanya Sesser ni binti wa miaka 23 ambaye alizaliwa akiwa na ulemavu wa kutokuwa na miguu, lakini yeye ni moja ya wanawake wajasiri zaidi Duniani ambao wameamua kuthubutu na kufanikiwa kujiweka kwenye njia ya kujiingizia pesa nyingi kupitia masuala ya fashion.
mode
Sesser alizaliwa Thailand, familia yake ilimtenga ndani ya kipindi cha wiki moja tu tangu azaliwe na kujikuta akilelewa mikononi mwa watu baki hadi alipofikisha umri wa miaka 15 na kujiingiza katika mambo ya mitindo kupitia kuzitangaza nguo za ndani za wanawake.
mode4
Amesema hajutii kuzaliwa hivyo na kuamua kujihusisha na mitindo ambapo ameingia mkataba na makampuni makubwa kama Volcom, Nike na Rip Curl Girl… Mrembo huyu kwa siku anaingiza zaidi ya Dola 1000 ambazo ni zaidi ya Milioni mbili za Kitanzania.
mode6
Mbali na mitindo pia Sesser ni mwanariadha na sasa yupo katika maandalizi ya kushiriki mbio za walemavu zitakazofanyika Korea Kusini mwaka 2018.
mode11
Kanya Sesser akiwa na mlezi wake baada ya kutengwa na familia yake
mode7
mode2
juu

lov
Kanya Sesser akiwa na mpenzi wake Brian Waters


Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment