Friday, September 25, 2015

KOCHA WA AFRICAN SPORTS AJIGAMBA , ATOA VISINGIZIO KIBAO


Tangakumekuchablog

Tanga, KOCHA Mkuu wa timu ya African Sports ya Tanga, Joseph Lazaro,amesema mapungufu ambayo yalikuwa yakiisumbua timu yake ameyarekebisha na iko tayari kuvaa Ndanda Jumapili.

Akizungumza wakati wa mazoezi ya timu yake jioni hii uwanja wa Mwakidila, Lazaro alisema kulikuwa na mapungufu sehemu ya ufungaji na beki ila kwa sasa amelirekebisha.

 “Mapungufu ambayo timu yangu ilikuwa ikisumbuka nayo nimeyarekebisha na sasa niko tayari kwa pambano la Ndanda----matokeo ya nyuma washabiki wa African Sports sasa wasahau” alisema Lazaro na kuongeza

“Tulikuwa na tatizo la beki na ufungaji jambo ambalo lilikuwa tatizo na kupata matokeo mabaya----kila kitu sasa kiko sawa na niwatake washabiki wetu waje uwanjani kutushangilia kwa nguvu” alisema

Akizungumzia ligi msimu huu, kocha huyo alisema ni ngumu kutokana na timu zote kusajili wachezaji wazuri wenye uzoefu na mikimiki na wao kuchukulia kila mechi kwao ni fainali.

Alisema timu zote zimefanya usajili wanguvu na hivyo kuchukulia kila mchezo ambao uko mbele yao ni fainali kwani ukianza kusuasua mechi za mwanzo iko hatari ya mzunguko wa pili kupata matokeo mabovu.

“Ligi msimu huu ni ngumu na asikuambie mtu angalia timu zilivyofanya usajili wa nguvu----hii ni changamoto kwa kila timu na unatakiwa mechi saba umejiweka nafasi nzuri ya kusonga mbele” alisema Lazaro

Alisema kwa sasa vijana wake wanapata mazoezi ya nguvu na kuwadhhibiti katika kambi ya timu hiyo kuwajenga kisaikolojia na kimwili ili kupata ushindi kila timu inayokutana nayo.
                                              Mwisho




Wachezaji wa African Sports ya Tanga, wakifanya mazoezi uwanja wa shule ya Mwakidila kijiandaa na mchezo na Ndanda uwanjwa wa Mkwakwani Tanga Jumapili

No comments:

Post a Comment